Pages

Wednesday, January 17, 2018

DIWANI ALLY DAFFA ZIARANI SHULE YA SEKONDARI LUSHOTO


Akiambatana na Watendaji wa serikali na idara ya Elimu, Diwani wa kata ya Lushoto, Mhe. ALLY DAFFA leo alipata wasaa wa kutembelea shule na jumuiya nzima ya Lushoto Sekondari.


Akipokelewa na Mkuu wa Shule, mwalimu JENIPHER H. LAURICH, Mhe. Diwani aliambatana na Mtendaji kata ya Lushoto, Mhe. ALHAJI CHAMSHAMA, Afisa Elimu kata ya Lushoto, Mwalimu MSWAKI na Mwenyekiti na Mtendaji Kijiji cha Yoghoi, Mzee KADALA.


Dhumuni kuu la ziara hii ya Mheshimiwa Diwani na jopo lake, ni kukutana na Wazazi wa wanafunzi wote wa Lushoto Sekondari ambapo ajenda kuu zikiwa ni masuala ya Taaluma na Nidhamu shuleni miongoni mwa wanafunzi na kupanga mikakati ya jinsi gani ya kukza taaluma shuleni, ufaulu wa wanafunzi na vichocheo vya kufanyikisha ufundishaji na ujifunzaji ili  kuboreka zaidi. Kwa azimio la pamoja, Wazazi na ujumbe mzima wa viongozi hawa, wamekubaliana kuwepo kwa utaratibu maalum wa kupata chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni kwa muda wa masomo ili kuweza kukuza hali yao ya kujifunza, kupunguza utoro, uzembe na njaa wakiwa katika mchakato mzima  wa kupokea taaluma na kujifunza.

Pamoja na hayo, pia Watendaji waliwakumbusha Wazazi wajibu na majukumu yao katika masuala yahusuyo elimu, ikiwa ni pamoja na kuwasisitiza watoto wao kuhudhuria shule siku zote za masomo, kuwasimamia na kuwafunza tabia njema, kuwapa mahitaji yao ya kitaaluma na kufuatilia maendeleo yao ya shuleni.

Mara baada ya kikao na wazazi, Mhe. ALLY DAFFA alipata wasaa pia kukutana na Wanafunzi wote na kuongea nao mambo kadhaa ya kuzingatia kuhusu Taaluma, Nidhamu na maisha ya shule kwa ujumla. Masuala hayo kadhalika yalisisitizwa na Watendaji na Afisa elimu kata ya Lushoto.

Na mwisho walimu nao walipata kuongea na Mheshimiwa Diwani na Ujumbe wake, masuala kadhaa yahusuyo shule, kazi na jumuiya nzima ya wana Lushoto Sekondari.
Zifuatozo ni baadhi ya picha zikionyesha matukio ya ziara hii:

Mkuu wa shule ya sekondari Lushoto (mwenye nguo ya kitenge), Ms Jenipher H Laurich akiongea na wanafunzi kabla ya kumkaribisha Afisa Elimu Kata ya Lushoto Mwalimu Mswaki , kuongea na wanafunzi.


Afisa Elimu Kata ya Lushoto (mwenye suruari ya bluu; jukwaani) akiwa na Mkuu wa shule, Mhe. Diwani na Mtendaji kata ya Lushoto pamoja na baadhi ya walimu.




Mtndaji Kata ya Lushoto(mwenye suti nyeusi), Mhe. Alhaji Chamshama akiongea na wanafunzi.






Mhe. Ally Daffa, Diwani wa kata ya Lushoto, akizungumza na wanafunzi wa Lushoto sekondari. (kidato cha kwanza hadi kidato cha nne).










**************

No comments:

Post a Comment